Home Habari za michezo SIMBA NA MIPANGO MAALUM KWA MIQUISSONE

SIMBA NA MIPANGO MAALUM KWA MIQUISSONE

Habari za Simba

Uongozi wa Simba SC umeamua kumsuka Luis Miquisson ambaye ameanza kunoga kikosini amepewa ndinga kali ya kisasa, amehamishwa nyumba aliyokuwa amefikia pamoja na kukabidhiwa kwa mtaalamu spesho wa viungo kumnoa ili aendelee kumuweka fiti zaidi ya alipofikia sasa.

Habari zinasema kwamba Simba SC wamepania kuonyesha ukubwa na utofauti na mtani wao Young Africans, kupitia mashindano ya African Football League kwani tayari watani hao wote wako kwenye uwezekano mkubwa wa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Habari za uhakika zinasema kwamba tayari Luis yuko na mtaalamu huyo mwenye uzoefu mkubwa jijini Dar es salaam na mbali na kufanya naye programu za kawaida kwenye timu huenda mbali zaidi baada ya muda wa kawaida na atakuwa naye mpaka wiki ya tatu ya Oktoba.

Imedhihirika kwamba Luis amekabidhiwa ndinga ya kisasa aina ya Crown New Model ya mwaka 2023 ambayo inakadiriwa thamani yake ni zaidi ya Sh100 milioni na tayari juzi na jana ameonekana nayo kwenye matizi kule Bunju.

Mbali na ndinga amehamishiwa kwenye nyumba ya kifahari maeneo ya Mbezi Beach Africana ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba wa pande zote na vile vile kuhakikisha anatuliza akili uwanjani na kurejesha makali yake kwa klabu msimu huu.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AKUNA KICHWA AONA HAPANA........... SASA AMEKUJA NA HESABU HIZI