Home Habari za michezo HII NDIO FURAHI DAY SASA SINGIDA FG vs YANGA

HII NDIO FURAHI DAY SASA SINGIDA FG vs YANGA

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga SC, Ally Kamwe, amesema mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 12:30 jioni, umepewa jina la Furahi Day.

Kamwe amesema sababu za kuupa mchezo huo jina hilo ni kwa sababu wanataka mashabiki na wanachama wa Yanga kuja uwanjani na kufurahia soka safi.

“Tumeupa mchezo jina la FurahiDay kwa sababu tunataka mashabiki wetu waje wafurahi kwa kandanda safi siku ya Ijumaa.

“Ni siku ya mwisho ya kazi, hivyo stress zote za wiki unakwenda kuzitoa Benjamin Mkapa siku hiyo.

“Niwakaribishe sana Wanachama, Mashabiki na wapenzi wa Yanga kuja Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao.

“Tunataka tuweke rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuujaza Uwanja wa Mkapa kwenye mechi ya Ligi ambayo sio Derby.

“Ijumaa tutaanza jaribio hili la kuisaka rekodi hii, nawaamini sana mashabiki wa Yanga watalifanikisha hili,” alisema Kamwe.

SOMA NA HII  YANGA WAFUNGUKA UWEPO WA GAEL BIGIRIMANA KAMBINI