Home Habari za michezo MISHAHARA YA WACHEZAJI YANGA KULIPWA MASTAA SIMBA WAKISHINDA KESHO…MO DEWJI AFANYA KUFRU…

MISHAHARA YA WACHEZAJI YANGA KULIPWA MASTAA SIMBA WAKISHINDA KESHO…MO DEWJI AFANYA KUFRU…

Habari za Simba

WACHEZAJI wa Simba washindwe wao tu sasa hivi hiyo ni baada ya kuhakikishiwa kupewa pesa ya maana katika michezo miwili ya robo fainali ya AFL dhidi ya Al Ahly.

Simba Oktoba 20 wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo ya AFL dhidi ya Ahly utakaofanyika katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Ipo Hivi Simba kabla ya kuanza rasmi kwa michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 8 ndani ya Bara la Afrika walikabidhiwa bilioni 1 na CAF kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo.

Sasa taarifa ambazo zipo kutoka katika uongozi wa Simba ukipewa sapoti na Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’ umesema kuwa, utahakikisha fedha hizo ambazo wamezipata tayari kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo kutoka kwa wahusika wanaosimamia michuano hiyo wanawapatia kwa kiasi kikubwa wachezaji kama motisha kuelekea katika michezo yao hiyo miwili.

Taarifa za ndani zinadai kuwa , Simba imetenga Milioni 500 kwa ajili ya bonasi kwa mastaa wake kwa mchezo wa kesho tu, pesa hizo ni sawa au karibu na jumla ya pesa mastaa wa yanga wanazolipwa kwa mwezi na klabu yao.

Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Try Again alisema kuwa: “Tunachokizingatia katika michuano hii ni kwamba tunahitaji kufanya vyema hivyo tumeona katika pesa zile za maandalizi ambazo tumepewa na wasimamizi tunawapatia wachezaji ili wawe na morali nzuri.

“Ahly ni timu kubwa lazima sisi tuweze kuwa na mipango sawa katika kila namna, wachezaji lazima wawe katika hali nzuri ili waweze kufanya kazi yao bila kuwa na wasiwasi na tunaamini watafanya vyema,” alisema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  HUKU AKIWA NA DILI LA KWENDA MOROCCO, HUU HAPA MSIMAMO WA CHRIS MUGALU