Home Habari za michezo SIMBA IMESHAKUWA JANGA MO DEWJI AOGOPA KUFA KWA PRESHA

SIMBA IMESHAKUWA JANGA MO DEWJI AOGOPA KUFA KWA PRESHA

Baada ya Simba kufanikiwa kufanikiwa kufuzu kwa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia katika Uwanja wa Chamazi.

Wengi wameonekana kuwa na mashaka na kiwango cha timu hiyo ambayo kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa na ubora mkubwa katika Michuano ya CAF Afrika.

Simba imefanikiwa kufuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya kulazimiaha sare katika Dimba la Levy Mwanawasa ya magoli 2-2.

Hivyo sare ya mchezo wa jana inafanya matokeo kuwa 3-3 lakini Simba anakwenda Makundi kwa kuwa alipata magoli mengi ugenini.

Sasa mara baada ya mchezo kukamilika kwa sare ya bao 1-1 siku ya Jumapili Oktoba 1, Mwekezaji katika Klabu ya Simba SC Mohammed Dewji kupitia ukurasa wake wa X (twitter) ameandika;

“Dah, Jamani Simba Mtaniua na pressure”.

Unadhani kipi kimemsukuma tajiri kuandika andiko hilo? Tupe maoni yako

SOMA NA HII  ROBERTINHO AIBUKIA YANGA AMPA GAMONDI MBINU ZA KUIUA AL AHLY