Home Habari za michezo HALI YA KWA MKAPA IKO HIVI MUDA HUU SIO POA

HALI YA KWA MKAPA IKO HIVI MUDA HUU SIO POA

HALI TETE UWANJA WA MKAPA…MVUA KUBWA YANYESHA UWANJA UMEJAA MAJI

KUTOKANA na hali ya hewa ya mvua, hakuna shamrashamra zilizozoeleka kwenye mechi za dabi za Simba na Yanga, ingawa haijazuia baadhi ya mashabiki kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Baadhi ya mashabiki wa timu hizo, wanatembeatembea nje ya uwanja huo, huku baadhi yao wakiendelea na biashara za hapa na pale ni kama vile wanasikilizia hali inakwendaje.

Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, inawafanya baadhi ya mashabiki kufanya kazi ya kutafuta sehemu za ‘kujistili’ wengine wakiendelea kunyeshewa na hawaonyeshi kujali hasa wale mashabiki ambao wanapiga mavuvuzela.

Wakati huo huo, wafanyabiashara ya miamvuli, wanaonekana kutumia fursa hiyo kuwauzia watu waliofika uwanjani hapo hasa wale ambao hawataki kuloa na mvua.

Kwa upande wa askari wa kulinda usalama nao wanaonekana kusimama kwenye baadhi ya maeneo kama getini ingawa hawana presha yoyote ya kukumbana na kashikashi za watu wanaotaka kuingia uwanjani.

  1. Leo saa 11 jioni itapigwa mechi ya Ligi Kuu Simba dhidi ya Yanga katika uwanja huo wa Mkapa

SOMA NA HII  KOCHA MPYA WA YANGA AWEKA WAZI MIPANGO YAKE, ATAJA SIFA ZA WACHEZAJI ANAOWATAKA