Home Habari za michezo HIZI HAPA SABABU ZA YANGA KUWA JUU YA MAMELOD SUNDOWNS KWENYE VIWANGO...

HIZI HAPA SABABU ZA YANGA KUWA JUU YA MAMELOD SUNDOWNS KWENYE VIWANGO VYA SOKA..

Habari za Yanga SC

Nimeona maswali ya watu wengi wakihoji kwanini Yanga wamekaa juu ya bingwa wa South Africa na Super league Mamelodi Sundowns, bila kusahau bingwa wa CAF confederation na Super Cup USM Alger.

Kimsingi IFFHS wako sahihi kutokana na vigezo vyao.

KIGEZO GANI HUTUMIKA KUPANGA ORODHA HIYO?

Ukiachana na vikombe IFFHS wanazingatia zaidi performance ya Vilabu husika kwenye mashindano yote yanayo tambilika na FIFA + CAF ndani ya mwaka mmoja.

Mfano huku kwetu Vilabu vyetu vinapimwa kupitia matokeo ya NBC premier league,Azam sports federation, CAF Champions league,CAF Confederation cup na CAF Super league.

Hapa yanakusanywa matokeo ya Vilabu vyote ndani ya mwaka mmoja kisha yanapigwa mahesabu na kupata idadi ya pointi….atakaye kuwa na idadi kubwa atakaa juu ya mwenzake.

Kila ushindi kwenye mechi zinazo tambulika FIFA na CAF unapewa alama (4) na sare inahesabika alama (2)

Kimsingi ukitazama Form ya Mamelodi na USM Algier ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Novemba 1, 2022 to Oktoba 31, 2023 utagundua Yanga wameshinda mechi nyingi kwenye mashindano yote kuliko hawa wamba wawili.

Mfano msimu uliopita USM Alger walimaliza nafasi ya 11 kwenye ligi ya kwao hivyo ni wazi walipoteza mechi nyingi sana.

Yes Mamelodi walitwaa ubingwa wa kwao lakini ukiangalia form yao wana sare zaidi ya nane kwenye mashindano yote bil kusahau vipigo kadhaa mbele ya TS Galaxy, Orlando Pirates n.k.

Ila wao Yanga wana sare chache na vipigo kidogo ukilinganisha na hawa wamba wawili.

SOMA NA HII  GAMONDI AFICHUA SIRI YA KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI ZA NDANI