Home Habari za michezo ILE ISHU YA ZRANE KURUDI SIMBA UKWELI WOTE HUU HAPA….KIGOGO AFUNGUKA A-Z...

ILE ISHU YA ZRANE KURUDI SIMBA UKWELI WOTE HUU HAPA….KIGOGO AFUNGUKA A-Z ISHU ILIVYO…

Habari za Simba SC

WAKATI tetesi zikieleza kuwa jina la Adel Zraine aliyewahi kuwa kocha wa viungo wa Simba lipo mezani, bosi ndani ya timu hiyo kafunguka kuhusu kurejea kwake kuanza kazoo majukumu mapya.

Ikumbukwe kwamba nafasi ya kocha wa viungo ipo wazi baada ya aliyeanza na timu msimu wa 2023/23 Corneille Hategekimana aliyesitishiwa mkataba wake Novemba 7.

Mbali na kocha wa viungo timu hiyo ipo chimbo kumsaka kocha mpya atakayechukua mikoba ya Roberto Oliveira ambaye alisitishwa mkataba wake ndani ya timu hiyo.

Meneja wa Idara ya habari na mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa ni suala la muda kutambua nani atakuwa nani katika kikosi hicho.

“Adel amekuwa akitajwa mara nyingi tunapokuwa hatuna kocha wa viungo. Ukweli ni kwamba ni mwalimu mzuri lakini maamuzi yake yataamuliwa pale uongozi utakapokubaliana nani atakuwa katika nafasi ya kocha wa viungo.

“Atakapotambulishwa mwalimu mpya itakuwa rahisi kuweka kila kitu wazi kwa kuwa kuna mwalimu ambaye anakuja na watu wake na kuna mwalimu ambaye yeye yupo sawa kwa lolote litakalotokea hivyo tusubiri na tuone,” .

SOMA NA HII  SKUDU ATOA KAULI NZITO BAADA YA KUREJEA NCHINI