Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAARABU KESHO….BENCHIKHA NENO LAKE MOJA TU HILI HAPA…

KUELEKEA MECHI NA WAARABU KESHO….BENCHIKHA NENO LAKE MOJA TU HILI HAPA…

Habari za Simba

USHINDI ni kauli ambayo inazungumzwa na wanasimba pamoja na benchi la ufundi la Wekundu hao wa Simba, linaloongozwa na Kocha Abdallah Benchikha katika mchezo wa kesho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Simba kesho wanashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Wydad Casablanca, uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 10:00. Wekundu hao wakipata ushindi utaleta matumaini makubwa ya kwenda robo fainali ya ligi ya Mabingwa.

Timu hizo zinakutana kwa mara ya tano, ilianza kucheza 2011 Simba walipoteza mabao 3-0 mchezo uliochezwa nchini Misri na hivi karibuni walikutana mara tatu, mechi mbili Simba ilipoteza ugenini na kushinda uwanja wa Benjamin Mkapa .

Huu unakuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mara ya mwisho Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Jean Baleke.

Simba wanashuka kwenye mchezo huu wakiwa mkiani mwa kundi B wakiwa na pointi mbili baada ya kushuka uwanjani mara tatu wakipata sare mbili dhidi ya Asec Mimosas 1-1 na Jwaneng Galaxy bila kufungana huku ikiwa imefungwa 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca.

Kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha , alisema mchezo dhidi Wydad Cassablanca hautakuwa rahisi ni fainali yao hivyo wamejipanga wanashinda ili kuwafurahisha mashabiki wao ambao

Amesema ni mechi muhimu kwao wanapaswa kuwa imara ili wapate ushindi na kuweka matumaini hai ya kusonga hatua inayofuata.

“Wydad ni timu kubwa tumecheza nao Marrakech na kuonyesha mchezo mzuri nina imani na wachezaji wangu wataenda kujitoa ili tupate ushindi na kuwafurahisha mashabiki wetu.

Naenda kukutana Wydad yenye kocha mpya ambaye ni kocha mkubwa mzoefu lakini rafiki yangu namjua vizuri haitakuwa rahisi malengo yetu ni kushinda mchezo huu,”amesema Benchikha.

Amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa sapoti ili waweze kupata ushindi katika mchezo huo ambao umebeba matumaini yao kwenye hatua ya makundi.

Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein amesema wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huo ili waweze kujiweka katika mazingira mazuri.

“Huu ni mchezo muhimu kwetu kupata matokeo tunasahau yaliyopita na kuanza upya wachezaji wako vizuri tunaamini tutaenda kufanya vizuri kwenye mchezo huu,” amesema Mohamed Hussein.

Kocha Mkuu wa Wydad Casablanca, Faouzi Benzarti amesema mchezo utakuwa mgumu wamejiandaa kutafuta ushindi katika mchezo huo ambao ni muhimu sana.

Amesema wanaifahamu Simba vizuri na mechi ya mwisho katika uwanja huu walipoteza na wanakuja kivingine kuhakikisha wanashinda na kupata pointi.

“Tutaiheshimu Simba kulingana na ubora wao na ukizingatia mechi ya kwanza ilionyesha kiwango kuzuri na kuleta ushundani na kuweza kupata ushindi dakika za mwisho,” amesema Kocha huyo.

Naye mwakilishi wa wachezaji wa Wydad Casablanca, Moutie Yousse, amesema wanatambua ubora wa Simba kikubwa wanaenda kufuata kile ambacho walipewa katika uwanja wa mazoezi.

“Tumejiandaa vizuri, tunacheza kwa tahadhari kubwa kuhakikisha tunafanikiwa katika malengo yetu ya kupata ushindi katika mchezo wetu wa pili licha utakuwa wa ushindani mkubwa kwa sababu ya ubora wa Simba ,”amesema Yousse

SOMA NA HII  LEO NI SIKU YA KUMBUKIZI YA KULETWA DUNIANI JEMBE