Home Habari za michezo MASHINE MPYA YA MAGOLI SIMBA YAANZA ‘KUOMBA POO’ MAPEMA…

MASHINE MPYA YA MAGOLI SIMBA YAANZA ‘KUOMBA POO’ MAPEMA…

Habari za Simba leo

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Fredy Michael amesema ushirikiano kutoka kwa kila mtu ndani ya klabu hiyo itawasaidia malengo ya timu kufika haraka.

Amesema amefurahi kujiunga na timu na yupo na yupo tayari kuhakikisha anasaidia timu kufanya vizuri katika michezo iliyop mbele yao ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara, FA na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Freddy tayari amewasili nchini ikiwa ni mara yake ya kwanza kutua katika Ardhi ya Tanzania ni miongoni mwa wachezaji watano wapya waliosajili kipindi cha dirisha dogo akiwemo Babacar Sarr Saleh Karabaka, Ladack Chasambi na Edwin Balua.

Mshambuliaji huyo amesema Tanzania ni mara yake ya kwanza, amefurahi kuwa sehemu ya kikosi cha Simba na anaimani asataidia timu hiyo kushirikiana na wachezaji wenzake kufikia malengo.

Amesema ni ngumu kwa mchezaji mpya kuingia ndani ya timu na kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza lakini anaamini kwa ushirikiano atakaonyesha kwa wachezaji wenzake na kiwango atakachoonyesha anaimani atamshawishi kocha Benchikha (Abdelhak).

“Kikubwa ni ushirikiano kutoka kila mtu ndani ya klabu ikiwemo wachezaji wenzangu, nipo tayari kuipambania timu kusaidia inafikia malengo ambayo yanayotarajiwa.

Ninaimani kubwa ya kufanya vizuri na kukata kiu ya mashabiki, pia kutowaangusha kocha na viongozi walinisajili kwa ajili ya kuhitaji huduma yangu ili kufikia kile ambacho wanakitarajia kwenye mashindano mbalimbali yaliyopo mbele yao,” amesema Freddy.

Naye Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema wachezaji wote wasikuwepo katika majukumu ya timu ya Taifa wamewasili kambini na ikiwemo nyota wapya waliosajiliwa dirisha dogo kuanza mazoezi rasmi kwa ajili ya maandalizi ya michezo iliyopo mbele yao.

Amesema mazoezi walianza Gym baada ya kwenda uwanjani ilishindikana kutokana na mvua kubwa kunyesha na wanaendelea na program ya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo iliyopo mbele yao ikiwemo Ligi Kuu, Kombe la FA na mechi za kimataifa.

“Tumeshaanza mazoezi kwa wachezaji ambao hawako kwenye timu za Taifa, lakini tunatarajia hivi karibuni nao wataungana na klabu yao hasa kwa zile timu ambazo zimetolewa katika AFCON,” amesema Kocha huyo.

Kikosi cha WekunduhaowaMsimbazi, kinachojifua katika uwanja wa Mo Simba Arena, wakijiandaa na mchezo wa Februari 17 na 23, mwaka huu, wakicheza dhidi ya Dodoma Jiji mchezo wa Ligi Kuu Bara, katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Asec Mimosas nchinu Ivory Coast mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  SHINDA MKWANJA KUPITIA DABI YA LONDON KASKAZINI