Home Habari za michezo ALLY KAMWE:- MATOKEO YANGA YANATUPA ‘STRESS’….

ALLY KAMWE:- MATOKEO YANGA YANATUPA ‘STRESS’….

Habari za Yanga

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa matokeo ya timu yao yanawapa stress kutokana na namna ambavyo timu yao imekuwa ikicheza kwa siku za hivi karibuni.

Kamwe amesema hayo juzi Alhamisi, Februari 8, 2024 wakati akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Mashujaa FC na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Itakumbukwa kuwa Yanga katika michezo mitatu imeshinda miwili na kutoa sare mchezo mmoja huku ikifunga mabao 3 tu na kufungwa bao moja. (Yaani 0-0 dhidi ya Kagera, 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji na 2-1 dhidi ya Mashujaa).

“Kila mechi tunayocheza ni kama fainali, na hili ndilo jambo linalotuumiza kichwa, kwa sababu lazima tutafute sehemu tu-make statement kwamba hii ni Yanga, hii ni timu kubwa, mambo ya kwenda kila mechi kama Ivory Coast yanatupa stress.

“Tunataka tuhakikishe mechi inayokuja kwenye mechi ya hafla ya miaka 89 ya Yanga, wachezaji wetu wakatupe burudani pale Sokoine Mbeya. Ila timu ya Ubingwa huonekana kwa staili hii kuna muda unayapata matokeo katika mazingira magumu kama haya.

“Kikosi chetu mmekiona, Ibrahim Bacca amerejea na leo amecheza, Bakary Mwamnyeto amerejea, Augustine Okrah amerejhea, Aziz Ki tayari yupo Dar, Djigui Diarra muda wowote atakuwa kwenye timu, kwa hiyo tunaamini tutakwenda Mbeya tukiwa na kikosi kamili na kumpa kocha Gamondi nafasi ya kuchagua kikposi cha kwanza.

“Haya ni mambo ya muda, kwenye ligi huwezi kucheza tu mechi zote bila kuwa na changamoto, lazima kuna nyakati kama hizi unapitia, lakini kikubwa tunashinda na kupata alama tatu. Mechi ijayo lazima tufanye zaidi ya hapa ili tutume ujumbe kwa kucheza vizuri na kupata matokeo mazuri,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  KUHUSU LOMALISA KUTAKA KUVUNJA MKATABA YANGA...UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA...