Home Habari za michezo A-Z YA WALIONYUMA YA GOLI 5-0 ZA YANGA vs IHEFU LEO...

A-Z YA WALIONYUMA YA GOLI 5-0 ZA YANGA vs IHEFU LEO HAWA HAPA….

Habari za Yanga leo

Stephane Aziz Ki amehusika katika mabao manne akifunga moja na kutoa asisti tatu wakati Yanga ikiendelea kusafisha njia ya kutetea ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kulipa kisasi kwa Ihefu FC kwa kuifunga mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Yanga imelipa kisasi hicho baada ya mzunguko wa kwanza ugenini kukubali kichapo cha mabao 2-1 mechi ambayo ndio pekee waliyoipoteza hadi sasa kati ya mechi 18 walizocheza, huku Aziz Ki akicheza soka la kiwango cha juu na kufikisha mabao 12 na asisti sita.

Kiungo Stephane Aziz Ki aendelea kufukuza mwizi kimya kimya hii ni baada ya kufunga bao lake la 12 na kumfikia kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye pia amepachika mabao 12 akitoa asist tatu kwenye ushindi wa mabao 4-0.

Ushindi wa Yanga umeifanya ifikishe pointi 49 baada ya kucheza mechi 18 wakiwaacha Azam FC kwa pointi tato ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zao 44 baada ya kucheza mechi 20.

Kwenye mchezo huo Yanga ilikuwa na mabadiliko ya kikosi eneo la kipa akirudi kipa namba moja Djgui Diarra akichukua nafasi ya Metacha Mnata, kiungo Pacome Zouzoua na Keneddy Musonda ambao walikosekana mchezo uliopita dhidi ya Namungo kwa sababu mbalimbali.

Mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa Yanga kutokana na kiungo Pacome kuongeza nguvu eneo la ushindani akiiandikia timu yake bao moja kwenye ushindi wa mabao 3-0 .

Bao la Pacome ni la saba, huku Mudathir ambaye pia kafunga bao moja ni bao lake la nane kwake msimu huu akimfikia Maxi Nzengeli ambaye pia kafunga mabao nane huku bao la Azaz Ki ambalo ametupia dakika ya 61 amemfia Fei Toto.

Mchezo kipindi cha kwanza ulianza kwa Yanga kuonekana kuhitaji mabao zaidi wakiwashambulia wapinzani wao Ihefu FC mara kwa mara huku wapinzani wao wakionekana kukubali kuingia kwenye mfumo na kuwaacha Yanga wakiutawala mchezo.

Yanga ilipata mabao mawili kipindi cha kwanza wakitumia dakika tisa kuandika bao la kwanza lililofungwa na Pacome huku bao la pili likifungwa dakika ya 29 na Mudathir mabao yalidumu hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika.

Kipindi cha pili Ihefu FC walionyesha mabadiliko kwa kucheza kwa kushambulia lango la Yanga zaidi ya mara tatu lakini mashambulizi yao hayakuzaa matunda kutokana na kukosa utulivu ndani ya boxi.

Yanga licha ya kuongoza kwa mabao mawili bado walikuwa na uchu wa kuendelea kupachika mabao dakika ya 68 Aziz Ki alikwamisha mpira nyavuni akiifungia yanga bao la tatu na la 45 kwa timu yake kwenye mechi 18 walizocheza.

Dakika ya 85 mabadiliko ya Miguel Gamondi aliyemtoa Mudathir Yahya na kumuingiza Agustin Okrah aliifungia Yanga bao lake la kwanza na la tano kwa timu yake bao ambalo lilidumu hadi kipyenga cha mwisho cha mwamuzi kuashiria kuisha kwa mpira.

Bao la Maxi kwa mujibu wa maamuzi ni bao lakini halijaingia kwenye mstari wa mwisho wa kuashiria ushindi lakini mwamuzi wa kati alithibitisha kuwa ni bao.

Ihefu imeingia kwenye rekodi ya timu tatu zilizofungwa mabao matao baada ya Simba kukubali 5-1, KMC 5-0, JKT Tanzania 5-0 na wao leo 5-0.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI