Home Habari za michezo KISA ISHU YA ‘MAJINI NA WACHAWI’….MAYELE NA MORRISON WATUPIANA MANENO …

KISA ISHU YA ‘MAJINI NA WACHAWI’….MAYELE NA MORRISON WATUPIANA MANENO …

Habari za Michezo

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya FAR Rabat ya Morocco ambaye ni raia wa Ghana, Bernard Morrison na mshambuliaji wa Klabu ya Pyramids FC ya Misri, raia wa Congo DR, Fiston Mayele wameibua jambo mtandaoni.

Hii ni baada ya Morrison ambaye amewahi kuchezea Yanga, kupitia ukurasa wake wa Instagram kuandika;

“Sio kwa sababu niliacha kutumia magongo utanitumia Majini. Nitawapeleka tu Zanzibar na watasahau hata ni Majini. Imagine Ghost smoking shisha utaenjoy wallah.”

Baada ya Morrison kuandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram mshambuliaji wa Pyramids, Fiston Mayele ambaye amewahi kuichezea Yanga pia wakiwa pamoja na Morrison, amekuja kwenye post hiyo na kuandika;

“Come back to Morocco are looking for you there witch.” Kwa tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi “Rudi Morocco wanakutafuta wewe mchawi”

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni Mayele aliingiabkwenye mzozo na mashabiki wa Yanga akidai kuwa wamemtupia majini ndiyo maana hafungi mabao siku hizi.

SOMA NA HII  IMEFICHUKAAH....MSHAHARA WA KOCHA MPYA SIMBA NI KUFRU....KULIPWA ZAIDI YA MIL 50 KWA MWEZI...

1 COMMENT