Home Habari za michezo BAADA YA PACOME KWENDA SAUZI NA YANGA….GAMONDI ‘KAJILAMBA MDOMO’…KISHA AKASEMA HILI..

BAADA YA PACOME KWENDA SAUZI NA YANGA….GAMONDI ‘KAJILAMBA MDOMO’…KISHA AKASEMA HILI..

Habari za Yanga leo

BAADA ya kurejea kikosini Pacome Zouzoua akipona kwa asilimia 100, Kocha Mkuu Miguel Gamondi ameahidi kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake kuelekea katika mechi ya marudiano ya robo fainali, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Memelodi Sundowns.

Jeshi lote la kikosi cha Yanga, akiwemo nyota huyo wameondoka nchini kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji wao Mamelodi Sundowns utakaochezwa Aprili 5, mwaka huu, uwanja wa Loftus Versfeld, Pretoria.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza timu hiyo iliwakosa Pacome, Khalid Aucho, Pacome Zouzoua na Yao Attohoula kwa sababu ya kuwa majeraha na kuukosa mechi hiyo uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kwa timu zote kutoka suluhu.

Kocha Gamondi amesema anamatumaini mkubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Amesema hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu ya mpinzani wake anafaida ya kucheza nyumbani lakinu anaingia katika mchezo huo kwa kuziba njia zote ambazo wapinzani wao wanaweza kupata ushindi.

“Ni kweli Pacome amerejea kukosini na yupo fiti ninamatarajio makubwa ya kufanya mabadiliko ya kikosi katika mchezo wetu wa maruadiano, Wachezaji wanatakiwa kumwaga jasho ili kupata matokeo mazuri.

Ukiwa na timu nzuri huwezi kuhofia mpinzani , malengo yetu makubwa ni kushinda mataji yote na kufanya vizuri zaidi, tunajua tunaenda kucheza na timu ya aina gani, licha ya kuzuia pia tunahitaji kushambulia,” amesema Gamondi.

Ameongeza kuwa Mamelodi Sundowns wazuri lakini amejipanga kukabiliana nao katika mchezo huo wa ugenini kupambana kuhakikisha wanafanikiwa kupata ushindi ugenini jambo ambalo kwenye mpira linawezekana.

Gamondi amesema kazi kubwa anayoifanya kwa siku chache kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake kutocheza kwa presha hasa safu ya ulinzi na ushambuliaji kuwa makini .

SOMA NA HII  MWL KASHASHA :- MUANGOLA WA YANGA BADO HAWEZI KUCHEZA LIGI YA BONGO

1 COMMENT

  1. Kila raheli timu ya wanaichi. Naitakia ushindi wa kishindo hapo April 5 dhidi ya wenyeji wao Mamelod. Daima mbele nyuma mwiko