Home Habari za michezo KUHUSU KIFO CHA ADEL ZRANE..UTATA HUU HAPA….MANENO YAKE YA MWISHO UTALIA….

KUHUSU KIFO CHA ADEL ZRANE..UTATA HUU HAPA….MANENO YAKE YA MWISHO UTALIA….

Habari za Simba SC

KOCHA wa zamani wa viungo wa Simba, Adel Zrane amefariki dunia huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijafahamika.

Kwa mujibu wa klabu aliyokuwa akiifundisha kabla ya mauti kumfika, APR ya nchini Rwanda, imethibitisha kifo cha kocha huyo kupitia mtandao wa kijamii ‘Instagram’.

“Tunasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa kocha wetu wa viungo Zrane, sababu ya kifo chake bado haijafahamika. Pumzika kwa amani,” inasomeka hivyo taarifa ya APR.

Taarifa kutoka Rwanda zinadai kuwa, Adel pamoja na timu yake APR walikuwa na mechi Jumapili na alikuwa uwanjani kutimiza majukumu yake kama kawaida, kisha wachezaji na makocha wakepewa mapumziko ya siku moja yani Jumatatu.

Jumanne, dereva wake alienda anapoishi kwa lengo la kumchukua kama ilivyo kawaida, ambapo alimpigia simu mara kadhaa lakini simu yake haikuwa ikipokelewa.

Taarifa zinadai kuwa dereva huyo bila kuchoka aliendelea kupiga simu, na kugonga mlango bila kufunguliwa kwa muda mrefu, ikabidi awasiliane na mabosi wa APR ambapo walipofika walivunja mlango na kumkuta amelala kitandani kwenye hali ya umauti.

Vyanzo vyetu hapa Tanzania vinadai kuwa Adel alikuwa ni mnywaji wa pombe kali na mara nyingi wakati alipokuwa na Simba alikuwa anaungana na baadhi ya wachezaji kunywa haswa wakati wa mapumziko mafupi ya kazi.

Hali hii kama itakuwa aliiendeleza mpaka Rwanda, huenda ikawa ni chanzo endapo tu alichanganya pombe hizo kali na madawa mbalimbali ya kupooza au kuupa mwili nguvu.

MASTAA WAMLILIA
Wakimzungumzia kocha huyo wachezaji mbalimbali wamezungumzia nafasi waliyopata kushirikiana naye enzi za uhai wake, huku wengine wakionyesha tu kuumizwa na kifo chake.

Kiungo mkabaji wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga APR, Taddeo Lwanga ameposti picha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram na kuandika ‘Maisha ni mafupi, tumezungumza jana, sikufahamu kama utakutana na aliyekuumba leo. Pumzika kwa amani rafiki.”

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Singida Fountain Gate na sasa Namungo, Meddie Kagere ameandika ‘Ni habari mbaya pumzika kwa amani kaka yangu Zrane kila siku nitakukumbuka.”

Zrane ambaye alipita Simba akosaidiana na kocha mkuu Mfaransa Didier Gomes Da Rosa pamoja na aliyekuwa kocha wa makipa Mbrazili Milton Nienov kwa pamoja waliachana na timu hiyo baada ya kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu wa 2021-22.

Kabla ya kifo chake Zrane alipoondoka Simba aliandika: “Kwa masikitiko makubwa naondoka nchi niipendayo Tanzania. Yametimia. Muda umekwisha. Naipenda Tanzania nawatakia kila la heri watu wote na utawala wake.

“Tanzania itakuwa kimbilio langu la kwanza kwa likizo. Nawapenda wote na asante kwa misimu yote minne iliyopita. Mmekuwa familia yangu ya pili, nawapenda na kuwaheshimu wote.”

SOMA NA HII  UWEPO WA MAXI KOMBE LA MAPINDUZI KOCHA ATOA TAMKO HILI