Home Habari za michezo OHHHOOO….BENCHIKHA KAALIAMUA HUKO ….JOBE, FREDY, KIBU WAKIONA CHA MOTO….

OHHHOOO….BENCHIKHA KAALIAMUA HUKO ….JOBE, FREDY, KIBU WAKIONA CHA MOTO….

Habari za Simba leo

WAKATI Kikosi cha Simba kikiwasilini nchini Misri, Kocha Mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi, Abdelhak Benchikha ametumia siku tano kwa ajili ya kusuka safu yake ya ushambuliaji akiifundisha mbinu mbalimbali kuhakikisha kila nafasi watakayoipata dhidi ya Al Ahly kutoka nchini Misri, kuwa mabao.

Hatua ya Benchikha ni baada ya mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Al Ahly, uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, walitengeneza nafasi saba na kushindwa kuzitumia na wapinzani wao walipata moja na kupata bao 1-0.

Simba watakuwa kwenye Uwanja wa Kimataiga wa Cairo kesho kutwa Ijumaa kuwakabili Al Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika hatua ya robo fainali utakaochezwa kuanzia saa 5:00 usiku.

Kutambua umuhimu wa mchezo huo na kulingana na matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Al Ahly, Benchikha ametumia siku tano kwa ajili ya kuwapa mbinu na kuwakumbusha suala la umakini safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Fredy Michael, Pa Jobe Omar na Kibu Denis akiwataka kutokupoteza nafasi kizembe kwani mchezo huo ni wa maamuzi.

Mbali washambuliaji hao lakini pia kiungo wake, Clatous Chama, Fabrice Ngoma, Babacar Sarr , Saido Ntibazonkiza, Sadio Kanoute na Willy Essomba Onana kupewa maagizo maalumu kuelekea katika mchezo huo ambao kutafuta matokeo mapema na kutoruhusu bao.

Licha ya Benchikha kuendelea na mambo ya kiufundi, pia Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), ametoa ahadi nono kwa ajili ya wachezaji watakapofuzu na kucheza nusu fainali ya ligi hiyo.

Benchikha amesema baada ya mechi ya mkondo wa kwanza waliocheza nyumbani dhidi ya Al Ahly, walifanya makosa kwa kutotumia nafasi walizotengeneza.

Amesema baada ya mechi hiyo alianzia kufanyia kazi mapungufu ya kikosi chake kuanzia safu yake ya ushambuliaji kuwana makini na kuzitumia nafasi wanazotengeneza kugeuza na kuwa mabao hasa wakiwa ugenini.

“Tunahitaji kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kwa ajili ya kupata matokeo mechi kubwa, ninaimani kubwa kwa wachezaji wangu na kile nilichowapa katika uwanja wa mazoezi ndani ya siku tano tunaweza kufanya vizuri ugenini,” amesema kocha huyo.

Ameongeza kuwa walipoteza mchezo wa kwanza nyumbani na Al Ahly haikuwa malengo yao, anaimani mechi ijayo wanacheza kwa malengo makubwa ikiwemo kutumia nafasi zinazopatikana kuwa mabao kwa upande wao.

“Al Ahly timu kubwa ipo wazi na ina wachezaji wenye uwezo mkubwa nasi tunahitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa katika kuendeleza ushindani. Makosa ambayo tumefanya tumefanyia kazi kwa kuwa wachezaji wanafanya kazi kubwa kutimiza majukumu yao hilo linatupa nguvu kuamini kwamba tutafanya vizuri,” amesema Benchikha.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, amesema wao wawindaji na wameenda kushundana na kutafuta ushundi ugenini dhidi ya wenyeji wao Al Ahly.

“Tunaenda kukutana na timu tunayoijua, Kocha Benchikha amefanya kazi yake na viongozi tumemaliza majukumu yetu, katika kuhamasisha tunafanya vizuri katika mchezo wetu wa Ijumaa, Mwekezaji Mo Dewji ametoa kiasi kikubwa cha (hakuweka wazi) kazi kubwa ipo ya wachezaji wenyewe kupambana na kushinda mechi hii,” amesema Try Again.

Katika hatua nyingine Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kikosi kimewasili Misri leo saa 4:00 asubuhi na kesho wanaendelea kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya (Ijumaa) kuwavaa Al Ahly

Amesema kwa wachezaji wakiopo kwenye mipango ya kocha Benchikha wote wako fiti na hakuna mchezaja majeraha zaidi ya Aishi Manula ambaye alijitonesha kudonda alipokuwa katika majukumu ya timu za Taifa Stars.

“Baada ya uchunguzi wa jopo la madaktari, Manula ameumia katika eneo la paja ni pale alipoumia mara kwanza na kufanyiwa upasuaji, tumeshauriwa kipa huyo kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita kwa ajili ya matibabu na kupata muda wa kupumzika ili kuja kuwa fiti,” amesema Ahmed.

Kuhusu mechi dhidi ya Al Ahly, Ahmed amesema wamefanya maandalizi ya kutosha, Benchikha amerekebisha makosa na kutumia siku tano kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ijumaa

SOMA NA HII  HUO MKWARA WA SIMBA KWA ASEC SIO POA