Home Habari za michezo SIKU 7 KABLA YA KUKIPIGA NA SIMBA DAR….YANGA KUIVAA SINGIDA FG KININJA...

SIKU 7 KABLA YA KUKIPIGA NA SIMBA DAR….YANGA KUIVAA SINGIDA FG KININJA KESHO,…

Habarii za Yanga leo

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wanashuka dimbani kesho kusaka pointi tatu muhimu katika mchezo wa ligi hiyo dhidi ya wenyeji wao , Singida Fountain Gate FC katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote Yanga wakihitaji ushindi ili kuendelea kujihakikishia kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 52 na kuwaacha mbali kwa pointi walipo chini yake akiwemo Azam FC alama 49 na Simba (45).

Wakati Singida Fountain Gate FC wanahitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kusalia ndani ya ligi hiyo kwa msimu mwingine kwa sasa wakiwa wanafasi ya saba katika msimamo wakiwa na pointi 24.

Mechi tatu za mwisho walizokutana timu hizo, Yanga amefanikiwa kushinda zote, mchezo wa mzunguko wa kwanza Singida Fountain Gate FC amekubali kichapo cha mabao 2_0 ilikuwa ikiwa Oktoba 27, 2023.

Katika mchezo wa kesho Yanga wataendelea kukosa huduma ya wachezaji muhimu wawili, Yao Attohoula ambaye tayari ameanza mazoezi lakini hayupo katika mipango ya mechi hiyo na Pacome Zouzoua ambaye bado yupo katika program maalumu.

Kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema ameandaa kikosi chake vizuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kusaka pointi tatu dhidi ya wapinzani wao Singida Fountain Gate FC.

Amesema hakuwa na maandalizi mazuri katika mchezo wao wa kesho kwa sababu ya kutoka kwenye mchezo mgumu na safari hadi mwaka lakini wanahitaji pointi tatu muhimu.

“Nawaheshimu Singida Fountain Gate FC, tumefanya maandalizi mazuri cha muhimu ni kushinda mechi ya leo ili kuendelea kusalia katika uongozi wetu wa ligi hiyo,” amesema Gamondi.

Kocha Msaidizi wa Singida Fountain Gate FC, Ngawina Ngawina amesema wanacheza na timu kubwa wamefanya maandalizi mazuri na wako tayari kukabiliana na Yanga katika dakika 90.

Amesema wachezaji wana hali nzuri wamejipanga kusaka pointi tatu, wanafahamu ubora wa Yanga na kucheza kwa tahadhari kubwa kufikia malengo yao katika mchezo huo.

“Kwa misimu hii miwili Yanga iko vizuri kila mmoja analifahamu hilo, hatuwaogopi tunawaheshimuna na tutacheza kwa tahadhari kubwa kuhakikisha tunafanikuwa kuvuna pointi tatu muhimu katika mchezo wa leo,” amesema Ngawina.

SOMA NA HII  KOCHA WA AS VITA AKUBALI KUTUA YANGA