Home Habari za michezo SKAUTI SIMBA:- KLABU HAINA PESA YA KUSAJILI WACHEZAJI WA MAANA…

SKAUTI SIMBA:- KLABU HAINA PESA YA KUSAJILI WACHEZAJI WA MAANA…

Habari za Simba

Mashabiki wa Simba wanatamani kuona klabu yao ikisajili mastaa wa maana wanaong’aa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na hata Kombe la Shirikisho, hapa Mels anaeleza changamoto iliyopo:
.
“Simba inafuatilia hayo yote kupitia kazi yangu, wapo wachezaji ambao tumeshawachukua kutoka kwenye mashindano hayo lakini wengine wale bora zaidi. Mfano kumchukua mchezaji anayecheza kikosi cha kwanza cha Petro Atletico, Mamelodi unahitaji bajeti kubwa nadhani changamoto kubwa iko hapo, huyo mchezaji unayemuona kwanza analipwa fedha nyingi na yupo ndani ya mkataba, klabu yake itahitaji fedha nyingi, labda usubiri mpaka mkataba wake umalizike hapo unaweza kufanya kitu unaangalia hali ya klabu yako unakwenda kufanya uamuzi kwa maeneo ambayo unaona utayamudu.”
.
“Sio kitu rahisi kama ambavyo wengi wanadhani hasa unapoingia sokoni kutafuta mshambuliaji wa kati, mfano angalia Yanga baada ya kuondoka Mayele (Fiston) alikuwa mchezaji mzuri kwao alipoondoka akaletwa Konkoni (Hafiz) kumbuka alitoka ligi ya Ghana akiwa amefanya vizuri sana, lakini alipofika hapa akashindwa kuwa na muendelezo mzuri na sasa wamemuondoa.

Washambuliaji bora ni wachache sana, unaweza kumpata unayemuona bora ukakuta kuja nchi kama Tanzania anaona shida anataka kwenda Ulaya kwahiyo sio Simba pekee inasumbuka na hili, angalia Al Ahly ililazimika kwenda Borussia Dortmund kununua mshambuliaji Anthony Modeste kwa fedha nyingi, hii unaweza kupata picha ya ugumu wa kupata washambuliaji wazuri ulivyo.” — Skauti mkuu wa kusaka vipaji wa Simba, Mels Daalder.

SOMA NA HII  KWANINI MSUVA ASAINI YANGA...... HIZI HAPA SABABU 5 ZA YEYE KUFANYA IVO