Home Habari za michezo ENG HERSI:- NILIINGIA CHUMBANI CHA AZIZI KI NIKAMWELEZA ‘NAVYOMTAMANI’….

ENG HERSI:- NILIINGIA CHUMBANI CHA AZIZI KI NIKAMWELEZA ‘NAVYOMTAMANI’….

Habari za Yanga leo

Rais wa Klabu ya Young Africans, Hersi Said amefunguka mbinu alizotumia kuinasa saini ya kiungo Mshambuliaji Kutoka Burkina Faso, Stephen Aziz Ki aliyekuwa akinyatiwa na watani zao, Simba SC na baadhi vya Waarabu Kaskazini mwa Afrika.

Hersi ameeleza kuwa alisafiri hadi Morocco kwaajili ya kumuona Aziz Ki na ndipo urafiki na mawasiliano vilianza hadi kukamilisha dili lake la kutua Kwa Wananchi.

“Story ya Aziz ilianza muda mrefu, wakati huo Yanga haishiriki katika michuano ya kimataifa lakini Simba wako kimataifa na walikuwa group moja na Asec Mimosas na Aziz akaja kucheza hapa Dar akafunga, Aziz akawa anatajawa sana na wakati anatajwa alitajwa kwa muktadha wa kwenda Simba.

“Unawezaje kumshawishi mchezaji ambaye anashiriki michuano ya kimataifa kuja kucheza kwenye timu ambayo haina rekodi ya kufanya vizuri kimataifa? “Nilianza kumfuatilia Aziz nikatafuta namba zake nikazipata, nilishawahi kufunga safari hapa nikaenda mpaka Berkane, Morocco kwaajili ya kwenda kumuona Aziz akicheza kukutana nae na kujenga urafiki.

“Baada ya ile mechi kati ya Berkane na Asec nilienda hadi hoteli ya kina Aziz, wakati naongea nao nikajiiba nikaingia kwenye chumba cha Aziz Ki tukazungumza nikamwambia nina interest na wewe akaniambia umesafiri kutoka Tanzania hadi hapa kwaajili yangu? Nikamwambia ndio, palepale nikapata na namba ya Mama yake.

“Nikaanza kuwasiliana na Mama yake nikamwambia namtaka kijana wako nikaenda tena Ivory Coast nikapeleka Ofa yangu, ofa yangu ilikuwa ndogo kuliko ofa ambayo klabu za Sudan na Tanzania walikuwa wamepeleka kwa Aziz hapo sasa ndio tukaanza kuongea nikamwambia Mama Aziz nitamtunza Aziz kama mzazi,” amesema Eng. Hersi Said.

SOMA NA HII  SIO AL AHLY MLETENI YEYOTE, SIMBA WATAMBA