Home Habari za Simba Leo SABABU ZA KOCHA WA VIUNGO YANGA KUONDOKA…GAMONDI AHUSISHWA

SABABU ZA KOCHA WA VIUNGO YANGA KUONDOKA…GAMONDI AHUSISHWA

Habari za Yanga Leo

KLABU ya Yanga inasemekana kuachana na kocha wa viungo wa timu hiyo, Youssef Ammar ambaye amedumu katika klabu hiyo kwa mafanikio makubwa sana.

Kocha huyo alifanya mahojiano na kuelezea namna ambavyo mkataba wake ulivyoisha na aliyelazimisha aondolewe kwenye benchi la ufundi la Yanga, ni kocha mkuu wa klabu hiyo.

“Kwa bahati mbaya mkataba wangu na Yanga umemalizika, na Yanga hawawezi kuongeza mkataba na mimi”

“Yalikuwa ni maamuzi ya upande mmoja, maamuzi hayakuwa kwa asilimia 100% kutoka Yanga bali uongozi wa Yanga umelazimishwa kufanya haya maamuzi na yamefanywa na mkuu wa benchi la ufundi Kocha Gamondi.”- Youssef Ammar, Daktari.

Miguel Gamondi anaelezwa kufanya mapendekezo yake ya wachezaji anaowahitaji msimu ujao, na kwa wachezaji ambao hawezi kuwatumia katika kikosi hicho.

Ipo wazi sasa aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube, atajiunga na Yanga msimu huu, kila kitu kinafanyika kwa umakini mkubwa ili makubaliano ya kusaini mkataba na nyota huyo wa Zimbabwe akipige Yanga.

Mapema hii leo Kiungo wa Yanga Aziz Ki alisikika akivujisha usajili huo alipokuwa anapiga story na timu ya habari ya klabu hiyo,Priva Abiud Shayo Maarufu kama Privadinho, na Abdulraziz.

Aziz Ki alisema “Mimi sitaki kuwa mfungaji bora, Dube anakuja kuna Guede kwenye timu yetu”

Kwa kauli hii ya Aziz Ki inatosha kuthibitisha zile tetesi za mshambuliaji huyo aliyeachana na Azam FC kwa aina yake, kesi ambayo ilifika hadi TFF.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI vs AL AHLY KESHO... SIMBA WAFANYA MAAMUZI HAYA MAGUMU...