Home Habari za Simba Leo SAFARI YA ABDULRAZACK HAMZA KUTOKA AFRIKA KUSINI…HADI SIMBA

SAFARI YA ABDULRAZACK HAMZA KUTOKA AFRIKA KUSINI…HADI SIMBA

HABARI ZA SIMBA, AbdulRazack Hamza

UONGOZI wa Klabu ya Simba Julai 4 jana ulitangaza usajili wa beki wa kati Abdulrazack Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka miwili.

Simba SC ilimtambulisha mchezaji huyo mida ya mchana, ikiwa ni muendelezo wa hatua ya kuwatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na Michuano ya Kimataifa.

Taarifa ya Simba iliyochapishwa kwenye mitandao yake ya kijamii inasema kuwa Abdulrazack ana umri wa miaka 21, bado ana nguvu na muda mrefu wa kucheza soka.

β€œAbdulrazack ana umri wa miaka 21 bado ana nguvu na muda mrefu wa kucheza soka na tunaamini atakuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi chetu.

β€œAbdulrazack ni mchezaji kijana wa Kitanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini kwa ubora mkubwa akiwa kwenye kikosi cha kwanza.

β€œUkiacha ubora alionao na umri wake ni mchezaji ambaye anaijua vizuri Ligi ya Tanzania kwa kuwa amecheza kwa ubora katika timu za Mbeya City, KMC na Namungo FC,” imeeleza taarifa hiyo ya Simba SC.

Lakini huenda wengi wakawa wanajiuliza kijana huyu kwa umri wake mdogo imekuaje akacheza timu zaidi ya tatu na hadi kutimkia Afrika Kusini.

Safari ya maisha ya Abdulrazack Hamza ilianzia katika Akademi ya michezo ya klab ya Azam FC mwaka 2017 akiwa timu ya vijana chini ya umri wa 17.

Mwaka 2021 klabu ya Mbeya City ilikuwa inashiriki Ligi Kuu kipindi hicho ya moto kabisa, ilimsajili kijana na kumpaΒ  Β nafasi ya kuonesha uwezo wake, kisha mwaka uliofuata akajiunga na KMC FC ilikuwa ni 2022, mwaka 2023 akajiunga na klabu ya Namungo.

Nyota yake iling’aa MITHILI YAΒ  Almasi za Mwadui akaonekana na klabu a Super Sports ya Afrika Kusini, ikamsajili kijana ambapo alicheza kwa mafanikioΒ  makubwa.

Na sasa Simba ikaamua kumrudisha nyumbani ikimpa nafasi ya Kennedy Juma, awali usajili wa Lameck Lawi ulionekana kutosha lakini Simba imeona inapaswa kuongeza nguvu zaidi ya wazawa.

SOMA NA HII  KWA MARA YA KWANZA...NAHODHA YANGA AFUNGUKA SIRI HII YA KUWACHAPA RIVERS