Home Habari za Yanga Leo ALIYENYIMWA TUZO AZUNGUMZIA BAO LA BOKA

ALIYENYIMWA TUZO AZUNGUMZIA BAO LA BOKA

BEKI wa kulia wa KMC, Abdallah Said ‘T Lanso’ ameeleza ugumu wa kumkaba mlinzi wa Yanga, Chadrack Boka kwamba inahitaji kutumia akili na umakini wa hali ya juu. KMC jana ilikuwa ugenini katika Uwanja wa Azam Complex.

Huo ni mwendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Bara ikipoteza mchezo dhidi ya Yanga kwa bao 1-0 lililofungwa na Max Nzengeli katika dakika ya tano.

“Unapomkaba beki kama Boka unahitaji kuwa na utulivu na akili kubwa kutokana na kasi yake na ujuzi wa kupiga krosi, hivyo sikuwa na vita na yeye tu, bali kila mchezaji wa Yanga anapokuja eneo langu nilipewa maelekezo ya kuharibu,” amesema mchezaji huyo.

Katika mchezo huo beki huyo alikuwa na kiwango bora licha ya timu yake kupoteza akihakikisha anapunguza mashabulizi manne hatari pamoja na kutoa krosi zilizokuwa zinapigwa na Boka.

T Lanso amesema kiwango walichoonyesha ilikuwa ni mpango na maelekezo ya Kocha Abdihamid Moallin kuhakikisha wanawadhibiti washambuliaji wa Yanga na kupunguza mashambulizi langoni mwao.

Ameongeza kuwa kilichoonekana kumdhibiti Boka ni kwa sababu anacheza upande wake, hivyo hata angekuwa mchezaji yeyote angefanya hivyo.

“Jana tuliingia na mpango wa kuikaba na kuishambulia timu nzima ya Yanga kama ambavyo kocha alitaka tufanye na tulifanikiwa.

Tulikuwa tunashambulia kwa kuwashtukiza, lakini tulikosa umakini kidogo wa kumalizia kutokana na ubora wa wapinzani wetu,” amesema.

Hadi sasa KMC imecheza mechi sita za Ligi ikishinda mchezo mmoja dhidi ya KenGold kwa bao 1-0, sare mbili dhidi ya JKT Tanzania 0-0, Coastal Union 1-1 na kupoteza mitatu dhidi ya Azam 4-0, Singida Black Stars 2-1 na Yanga 1-0.

SOMA NA HII  MCHAWI WA SIMBA APATIKANA