Home Habari za Simba Leo KWA HAMZA WA SIMBA, KIPIMO BORA NI DUBE,BLANCO, & BALAKE

KWA HAMZA WA SIMBA, KIPIMO BORA NI DUBE,BLANCO, & BALAKE

HABARI ZA SIMBA- HAMZA

MCHAMBUZI wa michezo wa EFM na TV E amesema kuwa kitasa wa Simba Abdulrazack Hamza aliyeonesha uwezo na kiwango kizuri katika mechi mbili za Tabora Utd na Fountain Gates.

“Kijana wa miaka 23 AbdulRazack Hamza ‘Spear Jr’ mlinzi wa kati wa Simba ameendelea kuonyesha kiwango kizuri tangu aanze kupewa nafasi na Kocha Fadlu Davids.”

“Kwa umri wake hii hazina kwa Taifa hasa wakati ambao tutawania kufuzu AFCON ya 2025 na baadae kuwa wenyeji katika Afcon ya pamoja ya Afrika Mashariki mwaka 2027.”

“Michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Tabora Utd na Fountain Gate ameonyesha wazi kuwa akipewa nafasi zaidi atakuwa msaada kwa Simba.”

“Binafsi nitampima zaidi ubora akikutana na washambuliaji kama vile Prince Dube,Jhonier Blanco,Jean Bakeke na washambuliaji wengine katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC).”

Alimalizia kwa kusema “SIWAWADHARAU MASTRAIKA WA TABORA NA FOUNTAIN GATE FC”

SOMA NA HII  KISA SIMBA 'KUFELI' MSIMU HUU....CHAMA AMTUPIA LAWAMA KOCHA MRAZILI...ADAI YEYE NDIO CHANZO..