Home Habari za michezo SIMBA NA YANGA CAF WANATAMANISHA.

SIMBA NA YANGA CAF WANATAMANISHA.

Habari za Simba na Yanga

WAWAKILISHI PEKEE wa Tanzania kwa upande wa Kimataifa, Simba na Yanga wanakabiriwa na michezo ya raundi ya pili kufuzu hatua ya makundi, wote watakuwa ugenini kabla ya kurudi Benjamin Mkapa umalizana na wapinzania wao.

Yanga anayeshiriki Klabu bingwa Afrika, atacheza na CBE ya Ethiopia huku Simba atasafiri hadi Libya kukipiga na Al Ahli Tripoli Septemba 15 Jumapili.

Kufanya vizuri katika mechi hizo kutazifanya Yanga na Simba zijihakikishie kutinga hatua ya makundi kwenye kila shindano ambalo kila moja ipo kwa upande mwingine ikiziweka katika nafasi nzuri ya kuongeza idadi ya pointi kutokana na ushiriki wao kwenye mashindano hayo ya klabu na hivyo kuzidi kupanda katika chati za ubora za klabu za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf).

Yanga itakuwa katika nafasi nzuri ya kukusanya idadi kubwa ya pointi kwa vile timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika inapata idadi kubwa ya pointi kutokana na mafanikio inayofikia kuanzia hatua ya makundi kulinganisha na zile za Kombe la Shirikisho Afrika ambazo hazipati pointi nyingi labda tu zinapofanikiwa kuingia nusu au fainali.

Kwa chati ya sasa ya Caf, Simba iko nafasi ya saba ikiwa imekusanya pointi 39 na Yanga iko nafasi ya 13 ikiwa imevuna pointi 31.

Timu bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika inapewa pointi sita wakati inayotwaa taji la Kombe la Shirikisho Afrika inavuna tano. Mshindi wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika anapata pointi tano na kwenye Kombe la Shirikisho anapata pointi nne.

Inayoishia hatua ya nusu fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika inapata pointi nne na kwa upande wa Kombe la Shirikisho Afrika inapata pointi tatu.

Timu inayoishia robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika inavuna pointi tatu na katika Kombe la Shirikisho Afrika inakusanya pointi mbili huku inayomaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika inapata pointi mbili na kwa upande wa Kombe la Shirikisho Afrika inavuna pointi moja.

Pointi moja inapata timu ambayo inamaliza katika nafasi ya nne kwenye kundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na katika Kombe la Shirikisho inapata pointi 0.5.

MAMILIONI YANUKIA.

Kuingia hatua ya makundi ni zaidi ya kusaka heshima ya uwanjani kwani pia kutazifungulia milango ya fedha Yanga na Simba kupitia njia tofauti.

Njia ya kwanza ni fedha zitokazo Caf kama zawadi kwa kila hatua ambayo timu inaingia kuanzia ile ya makundi hadi fainali.

Kitendo cha kutinga tu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kinaihakikishia timu kiasi cha Dola 700,000 (Sh 1.8 bilioni) na ile inayoingia hatua ya robo fainali inavuna Dola 900,000 (Sh 2.3 bilioni).

Bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika anapata kiasi cha Dola 4 milioni (Sh10 bilioni), mshindi wa pili anapata kitita cha Dola 2 milioni (Sh 5 bilioni) na inayoishia nusu fainali inapata Dola 1.2 milioni (Sh3.2 bilioni)

Timu inayotwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika inapata kiasi cha Dola 1.5 miliono milioni (Sh4.1 bilioni) na inayoshika nafasi ya pili inapata Dola 1.4 milioni (Sh3.8 bilioni), Dola 600,000 (Sh1.6 bilioni) kwa inayoishia nusu fainali, kiasi cha Dola 300,000 (Sh816 milioni) kwa robo fainali, Dola 200,000 (Sh544 milioni) kwa nafasi ya nne kwenye kundi na inayoshika mkia katika kundi inapata Dola 100,000 (272 milioni) mtawalia.

Fedha nyingine ambazo Simba na Yanga zinaweza kuvuna ni zile za bonasi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye anatoa Sh 5 milioni kwa kila bao linalofungwa na klabu ya Tanzania inayoshiriki mashindano ya klabu Afrika.

SOMA NA HII  ILE SINEMA YA USAJILI WA KIUNGO MPYA MNIGERIA SIMBA IKO NAMNA HII AISEE...MWENYEWE KAFUNGUKA A-Z WANAOKWAMISHA DILI..

1 COMMENT

  1. […] hii Yanga na Simba zina mechi za kuamua hatma zao katika michuano ya kimataifa kila mmoja akipambania rekodi […]

Comments are closed.