Uncategorized

KOCHA YANGA AFICHUA SIRI YA MABAO YA KINDOKI

admin June 8, 2019 12:15 am


KOCHA wa magolikipa wa kikosi cha Yanga, Juma Pondamali amesema kuwa kikubwa kilichokuwa kinamponza mlinda mlango Klaus Kindoki kushindwa kufanya vizuri ni hofu akiwa langoni.

Kindoki ambaye ni chaguo namba moja mbele ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera msimu wa 2018/19 alikuwa akifanya makosa mengi ya kiufundi hali iliyofanya afungwe mabao kwenye baadhi ya michezo aliyokuwa langoni.

Mfano katika michezo ambayo alifungwa kwa makosa ya aina moja ni ule dhidi ya Mwadui FC uliochezwa uwanja wa Mwadui Complex ambapo alitema shuti alilopigiwa na Salum Ilanfya kabla ya Salum Aiyee kupachika bao, pia kwenye mchezo aliofungwa hattrick na Alex Kitenge alifanya makosa matatu ya kiufundi.

Pondamali amesema ni hofu tu ndiyo ilikuwa inamponza mlinda mlango huyo raia wa Congo.

“Ujue mlinda mlango ukiwa langoni ni lazima ujiamini, sasa Kindoki alichokuwa anafanya ni kushindwa kujiamini katika baadhi ya michezo hali iliyokuwa inasababisha anapoteza.

“Mlinda mlango ni makosa kuurudisha mpira ndani ya uwanja kama upo karibu na adui sasa yeye mpira ambao inabidi uukamate kwa mikono miwili yeye anautema kwa mikono miwili hali inayosababisha iwe rahisi kwa adui kufunga,” amesema.

TAIFA STARS: HAKUNA CHA KUHOFIA TUNAKWENDA KUFANYA MAAJABU SINGIDA UNITED WAJA NA MTINDO MPYA WA USAJILI, WATANGAZA FURSA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply