Uncategorized

LIPULI FC, KOCHA WAO MATOLA BADO HAKIJAELEWEKA KIANA

admin June 10, 2019 12:16 am


Uongozi wa Lipuli FC umesema kuwa bado haujakaa mezani kuzungumza na kocha, Seleman Matola juu ya kuongeza mkataba mpya kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Ofisa Habari wa Lipuli, Clement Sanga amesema kuwa baada ya ligi kuisha na kumaliza mchezo wa fainai kombe la Shirikisho walimpa mapumziko kocha pamoja na wachezaji.

“Kwa sasa bado hatujazungumza na kocha wetu Matola kwa kuwa baada ya kumaliza ligi pamoja na mchezo wetu wa FA tulimpa mapumziko hivyo muda ukikamilika tutamuita mezani kuyajenga.

“Amekuwa mwalimu bora ambaye msimu huu ametufanyia makubwa tunamheshimu na tunamuamini, kikubwa ninachojua bado ni mali yetu kwa kuwa hakuna taarifa mpya ambazo tumezipata juu yake licha ya kwamba tunajua lazima atakuwa anapigiwa mahesabu na timu nyingine,” amesema Sanga.

MANCHESTER UNITED KUMLIPA MKWANJA MREFU DAVID de GEA YANGA YAIKOMALIA SAINI YA NYOTA HUYU, IKITIKI BASI WANAKUWA NA VIUNGO WANNE MATATA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply