Uncategorized

DYBALA NJIA PANDA JUVENTUS KUELEKA MANCHESTER UNITED

admin August 1, 2019 2:38 pm

PAULO Dybala nyota wa Juventus na timu ya Taifa ya Argentina bado hajajua afanye maamuzi gani kwa sasa kama ni kutimka ndani ya kikosi hicho na kutafuta changamoto mpya ndani ya Manchester United.

Uongozi wa Juventus umesema kuwa ni wakati mzuri kwa nyota huyo kufanya maamuzi sahihi ili kuzuia maneno mengi ambayo yanasemwa juu yake kwa sasa.


Dybala amesema:-“Kuna ofa nyingi mkononi kwa sasa ambazo ninazitazama ila bado sijaona ipi ni bora kwangu kwa sasa, hivyo bado nasubiri wakati ukifika nitachukua maamuzi.

Nyota huyo ambaye amejiunga na Juventus msimu wa 2015/16 akitokea klabu ya Palermo ambapo alipachika jumla ya mabao 19 na assisti 8.

Msimu uliopita akiwa ndani ya Juventus alipachika mabao matano na assisti nne huku sababu za kushuka kiwango ikidaiwa kuwa ni utawala mpya wa Cristiano Ronaldo ambaye alijiunga na Juve akitokea Real Madrid.

AZAM FC LEO KUTESTI MITAMBO NA MASHINE HIZI MPYA KALI KINOMA BENETEZ KIBOKO YA GARETH BALE, CHEKI REKODI YAKE NDANI YA REAL MADRID

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply