Uncategorized

MANCHESTER UNITED NA CHELSEA LEO KITAWAKA, MAMENEJA WA TIMU ZOTE WALIKUWA WACHEZAJI WA TIMU ZAO

admin August 11, 2019 12:14 pm


MANCHESTER United leo itawakaribisha Chelsea kwenye mchezo wa kwanza ambao United inakuwa nyumbani Uwanja wa Old Trafford.

Agosti 11, leo Jumapili vumbi itatimka kwa wababe hawa wawili.

 
United itaingia uwanjani bila uwepo wa Erick Bailly ambaye atakuwa nje kwa miezi mitano akiuguza majeraha yake ya goti na pengo lake litazibwa na Harry Maguire.

Kwa upande wa Chelsea itamkosa Antonio Rudiger naye ana maumivu ya goti pamoja na Ruben Loftus na Hudson-Odoi huku N’Golo Kante ambaye bado hajawa fiti.

Timu zote mbili zinanolewa na makocha ambao wamewahi kuzichezea timu hizo kipindi cha nyuma.

Ole Gunnar Solskjaer, Meneja wa Manchester United amesema majeruhi kutokea hakuna anayepanga ila watacheza vizuri.

Frank Lampard, Meneja wa Chelsea amesema itakuwa kazi ngumu kuanza na United na mchezo utakuwa mzuri.

NEWCASTEL UNITED KUTUMIA AKILI LEO MBELE YA ARSENAL JESHI KAMILI LA AZAM FC LITAKALOANZA LEO DHIDI YA FASIL KENEMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply