Uncategorized

VODACOM WAREJEA LIGI KUU BARA KWA MASHARTI

admin August 17, 2019 7:56 am


Imeelezwa kuwa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom imekubali kudhamini tena Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao.

Vodacom ambao awali walijiondoa baada ya kutokuwa na maelewano baina yao na Bodi ya Ligi wamekubali kuweka kitita cha shilingi za kitanzania bilioni tatu.

Fedha hizo zinawekwa kwa masharti wakitaka timu nne zipungue kutoka 20 mpaka 16 ili kuendana na matakwa yao wanayoyataka,

Ikumbukwe katika misimu miwili iliyopita timu za Ligi Kuu ziliongezeka na kufikia 20 maamuzi ambayo yamechukua muda mrefu zaidi kufanyika.

Kuna uwezekano wadhamini hawa wakatangazwa leo katika mchezo wa Ngao ya Jamii baina ya Simba na Azam ama siku yoyote kuanzia leo.

MBRAZIL ALIYEKIPIGA NA NEYMAR JR, COUTINHO AMAPA TANO MBELGIJI WA SIMBA KAMPUNI YA SIMU, CHAKULA KUMWAGA FEDHA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply