Uncategorized

NGOMA AANZA KUNOGA SASA NDANI YA AZAM FC, ATUPIA KWENYE MECHI MBILI KWA HASIRA

admin September 6, 2019 9:18 am


DONALD Ngoma, mshambuliaji wa Azam FC ameanza kurejesha ushkaji wake na nyavu kwa kufanikiwa kufunga kwenye mechi zake zote mbili za kirafiki alizocheza.

Azam FC kwa sasa inajiandaa na mchezo wa kimataifa wa hatua ya Kwanza kwenye Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Septemba 15 uwanja wa Chamazi dhidi ya Triangle United ya Zimbabwe.

Kwenye michezo miwili ya kirafiki ambayo Azam FC wamecheza dhidi ya Transit Camp na Friends Rangers imeshinda kwenye mechi hizo kwa kutupia jumla ya mabao sita huku Ngoma akitupia mabao matatu.

Alianza kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Transit Camp uwanja wa Uhuru kabla ya jana kuongeza bao moja kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Frends Rangers uwanja wa Chamazi.

Mabao mengine matatu yaliyobaki mawili yalifungwa na Daniel Amoah na moja likifungwa na Idd Kipagwile.

YANGA WAIWASHIA MOTO BODI YA LIGI ISHU ZA ZAHERA KUPIGWA FAINI, TAMKO LAO HILI HAPA MAMA WA BEKI WA YANGA KUZIKWA LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply