Uncategorized

BOSI SIMBA AFUNGUKA JUU YA KUACHANA NA NYOTA TEGEMEO

admin January 11, 2020 9:36 pm

Uongozi wa klabu ya Simba umesema haujaachana na wachezaji wake Aishi Manula pamoja na Erasto Nyoni.

Kwa mujibu wa CEO mpya wa Simba, Senzo Mazingisa, ameeleza kuwa si kweli wameachana na wachezaji hao baada ya kuwa kwenye majeruhi hivi karibuni.

Akizungumza na Radio One, Mazingisa ameeleza bado wachezaji hao ni mali halali ya Simba na wataendelea kuwa nao siku zote.

Amefunguka kuwa wanaheshimu mchango wao na yanayoelezwa mitandaoni kuwa wameachana nao hayana ukweli wowote.

“Nyoni na Manula ni wachezaji wa Simba, hatujaachana nao kama inavyoelezwa.

“Sisi tutaendelea kuwa nao sababu kuwa majeruhi si chanzo cha sisi kuachana nao, yanayoandikwa yapuuzwe.”
YANGA YAZIDI KUNG’ARA KIMATAIFA, YAINGIA DILI NONO NA KAZIER CHIEFS UONGOZI YANGA WATOA TAMKO JUU YA UJIO WA JAMES KOTEI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply