Uncategorized

HIKI NDICHO KINACHOITESA KAGERA SUGAR KWA SASA NDANI YA LIGI

admin January 12, 2020 12:44 pm


KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa matokeo wanayoyapata kwenye ligi yanatokana na ushindani kuwa mkubwa wanajipanga kwa sasa kurejea kwenye ubora wao.


Kagera Sugar, jana ilipoteza mbele ya Polisi Tanzania kwa kufungwa mabao 2-1 uwanja wa  Ushirika, Moshi ikiwa imetoka kufungwa Coastal Union bao 1-0 uwanja wa Mkwakwani.

Maxime amesema :”Ligi ni ngumu na kila timu inapambana kupata matokeo chanya, hatuna mashaka na uwezo wa wachezaji makosa yetu tutayafanyia kazi,” amesema.

Mchezo wa ligi unaofuata kwa Kagera Sugar ni dhidi ya Yanga utachezwa Januari 15 uwanja wa Uhuru.
MOGELLA, MFAUME, MAYAY WASHIRIKI UZINDUZI DUKA JIPYA LA MICHEZO LA ANTA JESHI LA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE DHIDI YA BURUNDI UWANJA WA TAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply