Uncategorized

MZUNGU WA YANGA AWABADILISHIA MBINU WAPINZANI WAKE ADAI WACHEZAJI WAKE WAMECHOKA

admin March 7, 2020 3:05 pm

LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wanachoka kwa kucheza mechi nyingi mfululizo jambo ambalo analifanya ni kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake ili kuwapa muda wa kupumzisha akili kabla ya kuvaana na Simba, kesho, Machi 8,2020.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakicheza bila kupata muda wa mapumziko tangu usiku mwaka 2019 ambapo Desemba 24 walicheza na Mbeya City na kulazimisha suluhu.
“Tumekuwa na ratiba ngumu ambayo inabana tangu X-Mass, tulikuwa tunacheza na mechi zetu nyingi ni ngumu, kazi ninayofanya kwa sasa ni kuwapumzisha baadhi ya wachezaji ili wapate nafasi ya kupumzika,” amesema.
Wachezaji ambao wamekuwa wakipumzishwa mara kwa mara na Eymael ni pamoja na Mrisho Ngassa, Papy Tshishimbi, Mohamed Issa, Yikpe Granimien.
DE BRUYNE WA MANCHESTER CITY HATIHATI KUKOSA MANCHESTER UNITED YANGA YATUMA UJUMBE MZITO KWA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply