Uncategorized

REKODI ZAIBEBA YANGA LEO TAIFA MBELE YA KMC

admin March 12, 2020 10:24 am

LEO saa 10:00 Yanga itamenyana na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Yanga itaingia uwanjani ikijiamini baada ya kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka minne bila kuifunga Simba baada ya ushindi walioupata Machi 8 wa bao 1-0 kupitia kwa Bernard Morrison.

Rekodi zinaibeba Yanga mbele ya KMC kwa kuipoteza timu hiyo iliyopanda daraja msimu wa 2018/19 kwa kushindwa kusepa na pointi tatu kwenye mechi zote tatu za ligi walizokutana.

Yanga imeshinda mechi mbili msimu wa 2018/19 na sare moja kwenye mechi ya kwanza msimu huu 2019/20 kwa kufungana bao 1-1 walipokutana Uwanja wa Taifa.

KMC imeifunga Yanga mabao mawili huku yenyewe ikifungwa mabao manne ambapo mchezo wa kwanza kukutana ilipopanda daraja ilifungwa bao 1-0 kupitia adhabu ya faulo iliyopigwa na Feisal Salum mechi ya pili Yanga ilishinda mabao 2-1 na kuifanya isepe na pointi sita jumla na mechi yao msimu huu ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa anawaamini vijana wake watafanya kazi nzuri itakayowapa pointi tatu.
ALIYEMPA TABU AISHI MANULA WA SIMBA ATAJA KINACHOMFANYA ACHEKE NA NYAVU HIVI NDIVYO HASIRA ZA SIMBA KUFUNGWA NA YANGA ZILIVYOKUTANA NA SINGIDA UNITED UHURU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply