Uncategorized

SIMBA YAOMBA RADHI KISA KICHAPO CHA MABAO 8 WALICHOIPA SINGIDA UNITED

admin March 12, 2020 9:54 pm


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaomba radhi kwa mashabiki na timu ya Singida United kwa kuipa kichapo cha mabao 8-0 jambo ambalo hakutarajia litokee.

Simba ilishusha kichapo hicho, Machi 11 Uwanja wa Uhuru baada ya kunyooshwa na watani zao Yanga bao 1-0 Uwanja wa Taifa.

Sven amesema: “Tulikuwa tunahitaji ushindi lakini sio wa mabao mengi kama tuliyowafunga wapinzani wetu, hamna namna imetokea wanapaswa watusamehe kwani ni matokeo ndani ya dakika 90, wachezaji walitengeneza nafasi nyingi ila walishindwa kuzitumia kama wangefanya vema ingekuwa ni habari nyingine,”.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 kibindoni na imecheza mechi 28 ikiwa imefunga mabao 63.

KMC WATAJA KILICHOWAPA USHINDI MBELE YA YANGA IGHALO ALETA MATUMAINI MAPYA NDANI YA MANCHESTER UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply