Uncategorized

UONGOZI WA SIMBA WATAJA SABABU YA KUCHAPWA BAO 1-0 MBELE YA YANGA

admin March 12, 2020 8:24 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kichapo mbele ya Yanga kinawaumiza na wana kila sababu ya kukubali kuchapwa kutokana na makosa yao wenyewe.

Mara ya mwisho Yanga kuibamiza Simba ilikuwa ni mwaka 2016 wakati huo Kocha Mkuu alikuwa Hans Pluijm, raia wa Uholanzi.

Bao la Bernard Morrison limeibuka baada ya miaka minne kumeguka akifunga kwa adhabu ya faulo akiwa nje ya 18 na kumtungua Aishi Manula.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Masingisa amesema kuwa sababu kubwa ya wao kushindwa kupata ushindi mbele ya Yanga ni wachezaji wao kushindwa kujituma ndani ya Uwanja.


 “Kipigo kinaumiza na hasa ukizingatia kwamba tulijipanga kufanya vizuri, hakuna dabi nyepesi hivyo ni vigumu kupata matokeo kiwepesi, ili kushinda ni lazima wachezaji kujitoa kwa dakika 90 kupambana,” amesema.

ISHU YA KICHAPO CHA SIMBA KWA YANGA IMEISHA MAISHA LAZIMA YAENDELEE, WACHEZAJI JILINDENI UWANJANI ALIYEMPA TABU AISHI MANULA WA SIMBA ATAJA KINACHOMFANYA ACHEKE NA NYAVU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply