Uncategorized

SERBIA MAMBO BADO MAGUMU, CORONA YASIMAMISHA KILA KITU

admin March 20, 2020 8:01 am

NASORRO Mohamed nyota wa Tanzania anayekipiga kwenye Klabu ya OFK Zarkovo ya nchini Serbia inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza amesema kuwa kutokana na hofu ya kusambaa kwa virusi vya Corona shughuli zote nchini Serbia zimesimamishwa.
Nyota huyo ambaye alipata dili hilo akitokea klabu ya vijana ya Mtibwa Sugar alikwea pipa Februari 29 pamoja na Abdalah Shaibu ‘Ninja’ ambaye yeye anakipiga OFK Vyskor kwa mkopo baada ya kupewa dili la miaka miwili na Klabu ya MFK Vyskor.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mohamed alisema kuwa kwa sasa hakuna kinachofanyika ndani ya nchi ya Serbia kutokana na hofu ya virusi vya Corona.
“Huku tunamshukuru Mungu tupo salama ila hakuna kinachofanyika kwa sasa kwani hofu sio kubwa lakini shughuli zote zimesimama hivyo hakuna kinachoendela wakati huu,” alisema Mohamed.
KILICHO NYUMA YA SARESARE ZA TANZANIA PRISONS HIKI HAPA WACHEZAJI WAPEWA SOMO HILI LA KUFANYA WAKATI HUU BAADA YA KAMBI KUVUNJWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply