Uncategorized

KAGERE AFUNGUKIA KILICHO NYUMA YA MABAO YAKE

admin March 23, 2020 9:04 am


MTAMBO wa kutupia ndani ya Simba, Meddie Kagere amesema kuwa chanzo kikubwa cha yeye kufunga hat trick kwenye mechi zao ni kutokana na msukumo wa kutaka kufunga mabao mengi kwenye kila mechi.

Nyota huyo raia wa Rwanda amesema kuwa anapenda kutumia kila nafasi anayopata kufunga jambo linalomfanya aweze kufunga hat trick.

Msimu huu, Kagere amefunga hat trick moja mbele ya Singida United ambapo Simba ilishinda mabao 8-0 Uwanja wa Uhuru.


“Nikipata nafasi napenda kuitumia na kufunga kadri unavyofunga ndivyo unajiongezea nafasi ya kufunga zaidi ndio maana ninafunga kila ninapopata nafasi,”.

Msimu uliopita ambapo alimaliza akiwa amefunga mabao 23 alifunga hat trick moja mbele ya Coastal Union wakati Simba ikishinda mabao 8-1 Uwanja wa Uhuru.

NAMUNGO WABISHI KWELI, CHEKI WANAVYOKULA SAHANI MOJA NA YANGA MUUAJI WA SIMBA AMTAJA MKE WAKE KUHUSIKA KWENYE MABAO YAKE YOTE NDANI YA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply