Uncategorized

KOCHA YANGA: NINAJUA UJANJA WA WACHEZAJI WA AFRIKA, WATAKAOZEMBEA MAZOEZI YANGU NITAWAJUA

admin March 23, 2020 9:04 pm


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anajua ujanja wa wachezaji pale wanapopewa kazi ya kufanya huzembea jambo ambalo atalijua wakati watakapokutana kwenye mazoezi.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali ilisitisha kwa muda wa siku 30 shughuli zote za mjumuiko.

Eymael ambaye amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi 15 kwa sasa yupo zake Ubelgiji akiwa amepewa mapumziko ya muda na mabosi wa Yanga amesema kuwa ameacha programu maalumu kwa wachezaji wake.

“Nimeacha programu kwa wachezaji wangu na ninatambua tabia za wachezaji wa Afrika kwani nimefanya nao kazi ninajua kwamba wapo watakaozembea lakini nitawajua tukikutana kwenye mazoezi.

“Malengo yangu makubwa ni kuona kwamba wanakuwa bora muda wote ndio maana nimewapa programu hiyo endapo wataifuata itawasaidia kuwa bora na tutaendelea kufanya vema kwenye mechi zetu,” amesema.

HOFU YA WACHEZAJI KUPATA MAJERAHA YAONGEZEKA IWAPO LIGI YA ENGLAND ITAMALIZIKA JUNE 30 MZUNGU WA YANGA AMPA PROGRAMU MAALUMU ALIYEWABINA KAGERE NA BOCCO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply