Uncategorized

MTAMBO MMOJA WA SIMBA WAWAPOTEZA NYOTA TISA NDANI YA YANGA

admin March 23, 2020 10:04 pm

MABAO 19 ya mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere yamewapoteza nyota tisa wa kigeni wanaokipiga ndani ya Yanga kwa sasa.

Kagere akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo imesimamishwa kwa sasa, amefunga mabao 19 na kutoa pasi tano za mabao huku wachezaji wa kigeni wa Yanga kwa ujumla wamefunga mabao 18.

Nyota wa Yanga ambao wamesajiliwa ni pamoja na Bernard Morrison mwenye mabao matatu na ana pasi tatu za mabao, Yikpe Gnamien ana bao moja, Haruna Niyonzima ametupia bao moja huku Patrick Sibomana akitupia mabao matano na pasi tatu za mabao.

David Molinga ametupia mabao nane, Papy Tshishimbi, Lamine Moro, Erick Kabamba na kipa Farouk Shikalo hawana bao.

Simba imefunga mabao 63 ndani ya Ligi Kuu Bara kwenye mechi 28 huku Yanga ikifunga mabao 31 kwenye mechi 27.

MZUNGU WA YANGA AMPA PROGRAMU MAALUMU ALIYEWABINA KAGERE NA BOCCO KUMBE MABEKI SIMBA WALIKAMIA MCHEZO WAO MBELE YA YANGA, MSHAMBULIAJI ALIYEWAPA TABU ASIMULIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply