Uncategorized

HIMID MAO: VIWANJA VYA NDEGE VIMEFUNGWA KWA SASA HAKUNA RUHUSA YA KUTOKA

admin March 24, 2020 7:04 am


HIMID Mao, anayekipiga ndani ya ENPPI ya Misri amesema kuwa kutokana na Virusi vya Corona wamejifungia ndani na hakuna ruhusa ya kuondoka ndani ya nchi hiyo kutokana na safari za ndege kusitishwa kwa muda.

Kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Serikali nyingi zimechukua maamuzi ya kuzuia safari za ndege ambapo hata Tanzania pia hali hiyo imetokea.

Himid amesema:” Kwa sasa tunashinda ndani hakuna ruhusa ya kutoka nje ama kusafiri kutokana na kutokuwepo kwa safari za ndege ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.

“Hatuwezi kusafiri kwa sasa kutokana na viwanja kufungwa, vitu kwa ajili ya kula tulipata muda wa kununua na kuviweka ndani,” amesema.

CHAMA AKINUKISHA NDANI YA SIMBA, YUPO ZAKE ZAMBIA KWA SASA SIMBA YAIPOTEZA MAZIMA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply