Uncategorized

KILICHO NYUMA YA MAFANIKIO YA KAGERA SUGAR HIKI HAPA

admin April 16, 2020 11:31 am

MECK Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa kikosi chake kilikuwa kinabebwa na nidhamu pamoja na kujituma kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa ili kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema:”Tulikuwa katika kupambana kufikia malengo yetu na kilichokuwa kinatubeba ni ushirikiano wa kila mmoja ambapo wachezaji na benchi la ufundi letu lilikuwa ni moja.

“Kwa sasa burudani ya soka imekosekana kutokana na Virusi vya Corona hivyo ni muhimu kwa kila mmoja kuchukua tahadhari jambo ambalo ni muhimu na imani yangu Mungu atatufanyia njia katika hili tutapita salama.”.

Wakati Ligi inasimama Kagera Sugar ilikuwa imecheza mechi 29 ikiwa nafasi ya 8 kibindoni ilikusanya pointi 41. 

VIDEO: NAMNA YANGA ILIVYOJADILIWA BUNGENI HILI NDILO JEMBE ANALOLIKUBALI KOCHA MKUU WA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply