Uncategorized

CORONA YAVURUGA DILI LA KOCHA LIGI KUU

admin April 29, 2020 7:11 am


KOCHA Mkuu wa Namungo FC, Hitimana Thierry inaelezwa kuwa janga la Virusi vya Corona limetibua dili lake la kusaini kandarasi mpya.

Mkataba wa kocha huyo unafikia kikomo mwezi Juni jambo linalowafanya Namungo kutaka kumpiga pini mapema kabla ya fujo za timu nyingine kuanza kumpigia hesabu.

Ofisa habari wa Namungo FC, Kindamba Namlia amesema kama ingekuwa mlipuko wa janga la Virusi vya Corona wangekuwa wameshamaliza kazi.

🗣”Ni kweli mkataba na kocha Hitimana unaelekea ukingoni lakini tupo tayari kumuongezea mkataba mpya bado ni muhimu kwetu na kama isingekuwa hili janga la Corona angekuwa ameshasaini,” amesema.

Namungo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi zake kibindoni 50 baada ya kucheza mechi 28.

BEKI YANGA AKUBALI UWEZO WA MTUPIAJI NAMBA MOJA WA SIMBA KOSI KAZI LA NYOTA WA MTIBWA SUGAR ANAYEWINDWA NA YANGA LIPO NAMNA HII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply