Uncategorized

KLOPP ALIWAHI KULEWA CHAKARI MPAKA KUPOTEZA KUMBUKUMBU

admin May 13, 2020 4:11 am
JURGEN Klopp,  Kocha Mkuu w

a Liverpool amesema kuwa hakumbuki chochote juu ya Klabu ya Borussia Dortmund kutwaa ubingwa wa Bundesliga msimu wa 2011/12 wakati wa sherehe kwa kuwa alilewa chakari mpaka kupoteza kumbukumbu.

Klopp kwa sasa ni miongoni mwa makocha wenye majina makubwa duniani alitengeneza jina lake alipojiunga na Dortmund 2008 na ilipotwaa ubingwa walishangalia sana.

Klopp amesema kuwa furaha ilizidi kimo jambo lililomfanya anywe sana pombe na kupoteza kabisa kumbukumbu za namna sherehe za ubingwa zilivyokuwa msimu wa 2012.

Kwa sasa Klopp anapambana ndani ya Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England huku ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa pale ligi itakaporejea kwani imesimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona na taarifa zinaeleza itaanza Juni Mosi bila uwepo wa mashabiki uwanjani.

MILIONI 800 ZAFUMUA KIKOSI SIMBA NDANI YA GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO MSHAMBULIAJI WA ORLANDO PIRATES AKUBALI KUTUA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply