Uncategorized

MBALI NA KUPENDA KUKU WA BONGO KINGINE HIKI HAPA ANACHOPENDA MBRAZIL WA SIMBA

admin May 13, 2020 9:41 am


GERSON Fraga, raia wa Brazil nyota anayekipiga ndani ya Simba amesema kuwa miongoni mwa vitu anavyovipenda ndani ya ardhi ya Bongo mbali na kuku wa sekele ni pamoja na ukarimu wa watanzania.

Fraga anayependa kujiita mkata umeme amehusika kwenye mabao matatu ya Simba kati ya 63 ambapo amezitungua Coastal Union mabao mawili na KMC bao moja.

Kwa sasa zile purukushani za soka zimesimama kutokana na janga la Virusi vya Corona linaloivurugavuruga dunia ila kuna uwezekano ikarejea mwezi Juni.

Fraga amesema:”Tanzania ni nchi ya pekee kwani ukiachana na kuwa na chakula kizuri ambacho huwa napenda kula ikiwa ni wale kuku wa sekela pia watu wake ni wakarimu.”

MATUMAINI YAMEANZA KUONEKANA LIGI KUREJEA ILA KUNA UMUHIMU WA KUANZA MAANDALIZI MAMBO YAKIJIBU TU, KOSI MATATA LA SIMBA LITAKUWA NAMNA HII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply