Uncategorized

KIUNGO FUNDI WA SIMBA SASA KUIBUKIA YANGA, APIGWA MIAKA MIWILI

admin June 20, 2020 5:47 am


INAELEZWA kuwa kiungo wa zamani wa Klabu ya Simba aliyetwaa tuzo ya kiungo bora ndani ya Simba kwa msimu wa 2018/19 anaweza kuibuka muda wowte ndani ya Yanga kwa kuwa ni mchezaji huru.

Kotei alipomalizana na Simba aliibukia Klabu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini mambo yalipokuwa magumu akaibukia Klabu ya FC Slavia-Mozŕy ambako huko taarifa zinaeleza kuwa amevunja mkataba hivyo kwa sasa ni mchezaji huru.


Habari zinaeleza kuwa tayari Kotei ameshamwaga saini ya miaka miwili ndani ya Yanga kinachosubiriwa ni wakati wa kutambulishwa ndani ya Yanga.

Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga amesema kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa wakati wa usajili haujafika.

BUMBULI WA YANGA AFUNGUKIA UHUSIANO WAKE NA HAJI MANARA WA SIMBA GWAMBINA FC: TRASINT CAMP WANATUPA TIKETI KUSHIRIKI LIGI KUU BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply