Uncategorized

DILUNGA – MASHARTI YA MPENZI WANGU YAMENISAIDIA ..!!

admin June 23, 2020 3:00 pm

STAA wa Simba, Hassan Dilunga ‘HD’ amedai kwamba mpenzi wake pamoja na kocha wa sasa, Sven Vandenbroeck wamekuwa busta ya yeye kutamba Msimbazi.

Dilunga chini ya Patrick Aussems hakuwahi kupachika mabao kama ilivyo kwa Sven alikotupia manane sasa.

Dilunga alisema chini ya Sven amekuwa akimtumia zaidi kwenye eneo la kushambulia kuliko nyuma alikokuwa akimpanga Aussems.

Kuhusu mpenzi wake anasema; “Nilikaa na mpenzi wangu (amemficha jina)kabla ya msimu huu kuanza tulikubaliana kuwa anataka kuniona namaliza msimu nikiwa na mabao saba katika ligi jambo ambalo nililikubali na kumuahidi nitafunga mabao hayo na yatakuwa kama zawadi kwake.

“Nashuruku Mungu kabla ya msimu kumalizika nimelitimiza hilo baada ya kufunga katika mechi ya Mwadui juzi,” alisema.

“Kubwa ambalo nimefanikiwa katika malengo yangu ni kufuata maagizo ambayo napewa na Sven, ndio maana chini yake nimefunga mabao mengi zaidi na bado naendelea,” alisema Dilunga ambaye Simba imemuongezea mkataba wa miaka miwili.

MBELGIJI WA SIMBA ANAAMINI KUWA KIKOSI KIKIWA FITI WANASHINDA MECHI ZOTE SIMBA WAPIGA MATIZI YA MWISHO LEO, VITA YAO KESHO INA VIGINGI VIKALI MBELE YA MBEYA CITY

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply