Uncategorized

CHAMA CLATOUS AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA YANGA

admin July 14, 2020 6:47 pm


CLATOUS Chama, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hana hiyana iwapo atahitajika kukipiga ndani ya Yanga kwani kazi ya mchezaji ni kucheza mpira.

Chama amekuwa kwenye ubora wake msimu huu wa 2019/20 kwa upande wa kutengeneza pasi za mwisho ambapo anazo jumla 11 na amefunga mabao sita.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa Yanga inahitaji kupata saini ya nyota huyo ikiwa na lengo la kuboresha kikosi chao kwa msimu ujao.

Chama amesema:” Kwa mchezaji kazi yake ni kucheza bila kujali yupo wapi ila kikubwa ni utaratibu kufuatwa kwani kwa sasa nipo ndani ya Simba.

“Bado nina mkataba na Simba kwa timu ambayo itakuwa inahitaji saini yangu ni lazima iwasiliane na uongozi wa Simba,” amesema.

MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA, VITA YA KUSHUKA DARAJA IMEPAMBA MOTO YANGA YAWATAKA MASHABIKI KUSAHAU MATOKEO YA 4G MAISHA LAZIMA YAENDELEE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply