Uncategorized

COASTAL UNION:BADO TUTAZIDI KUPAMBANA, KESHO WANA KIBARUA MBELE YA KAGERA SUGAR

admin July 14, 2020 1:47 pm


BAKARI Mwamnyeto,  nahodha wa Klabu ya Coastal Union iliyo chini ya Kocha Mkuu,  Juma Mgunda amesema kuwa watazidi kupambana ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Beki huyo kipenzi cha Mgunda amekuwa Kwenye ubora wake msimu huu ambapo amekuwa kiongozi kwenye timu hiyo ambayo inaleta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.

Licha ya kuyumba hivi karibuni baada ya ligi kuendelea kwa kupokea vichapo vitatu mfululizo bado imesimama imara na kubaki nafasi ya tano.

Ilichapwa bao moja na Mbao FC Uwanja wa Kirumba, ikanyooshwa 1-0 mbele ya Alliance FC kisha ikakutana na kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Mbeya City pale Sikoine.

Kesho, Julai 15 ina kazi mbele ya Kagera Sugar Kaitaba iliyo chini ya Mecky Maxime aliyetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga.

Ipo nafasi ya tano Kwenye msimamo ikiwa na pointi 51 kibindoni baada ya kucheza mechi 34. Safu ya ulinzi imeruhusu mabao 27.

“Bado tutazidi kupambana kwani wapinzani wetu nao wanahitaji ushindi nasi tunahitaji pia ushindi,” amesema.

AZAM FC NA SIMBA SC ZAGONGANA KWA NYOTA HUYU MWILI JUMBA ANAYEKIPIGA MALAYSIA MWL .KASHASHA  – YANGA WALIKOSEA HAPA TU..!!!

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply