Uncategorized

YANGA YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA MWADUI FC TAIFA KWA KUFUNGANA BAO 1-1

admin July 18, 2020 6:47 pm

YANGA leo imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mwadui FC Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Julai 18.

Yanga ilianza kuandika bao la Kwanza dakika ya 27 kupitia kwa Feisal Salum ambalo lilidumu mpaka muda wa mapumziko.

Dakika 45 za kipindi cha Kwanza zilikamilika kwa Yanga kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa mbele kwa bao hilo la Fei Toto.

Kipindi cha pili Mwadui FC ilisawazisha kupitia kwa Yahya Mbegu dakika ya 56 na kufanya ubao usomeke 1-1.

Mwadui imeshindwa kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo wao uliopita wa Ligi na kuishia kuambulia pointi moja.

Yanga inafikisha pointi 68 huku Mwadui wakifikisha pointi 41 ndani ya Ligi wote wakiwa wamecheza mechi 36.

KESHO NDANI YA SPOTI XTRA JUMAPILI USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO KOCHA ANAYETAJWA KUIBUKIA SIMBA KUSHUKA NA JEMBE HILI LA KAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply