Uncategorized

MTUPIAJI NAMBA MOJA KWA WAZAWA ATAJA KINACHOMKWAMISHA

admin July 20, 2020 8:47 am


MTUPIAJI namba moja kwa wazawa ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Yusuph Mhilu amesema kuwa isingekuwa majeruha angefunga mabao mengi na kuleta ushindani kwa mtupiaji namba moja, Meddie Kagere.

Mhilu ametupia jumla ya mabao 13 akiachwa kwa mbali na Kagere raia wa Rwanda  mwenye mabao 22 akiwa ni namba moja kwa sasa kwa utupiaji. 

Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa amekuwa akishindwa kuendeleza moto wake ndani ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.

“Namshukuru Mungu nimekuwa nikipata nafasi ya kucheza na kufunga ninafunga ila nina amini isingekuwa kusumbuliwa na majeruhi ningekuwa nimefunga mabao mengi kwa ajili ya kutimiza wajibu wangu ndani ya timu.

“Ila kwa kuwa nimekuwa nasumbuliwa na majeruhi imekuwa ikinipa wakati mgumu kufikia malengo ambayo nimejiwekea ila nina amini bado uwezo ninao,” amesema.

Mhilu kwa sasa anatibu majeraha ya nyama za paja aliyopata hivi karibuni kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 kwa sasa amesema anaendelea vizuri.

BALAMA NA NIYONZIMA NDO BAS TENA MSIMU HUU NDANI YA YANGA MASHABIKI WA SIMBA KUPIGA PICHA BURE NA KOMBE NI HASARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply